KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, January 12, 2011

Mgogoro wa Lebanon waichanganya Marekani

Hariri alipokutana na Obama kabla ya kufupisha ziara yake

Kuanguka kwa serikali ya Waziri mkuu Saad Hariri nchini Lebanon, kunaongeza hesabu katika orodha ya changamoto zinazoukabili utawala wa Marekani wa rais Barack Obama katika Mashariki ya kati.
Rais wa Iran alipoizuru Lebanon mwaka jana wakati mvutano ukizidi kati ya Hezbollah na MarekaniMtaalamu wa kanda hiyo katika chuo kikuu cha Oklahoma nchini Marekani

Sambamba na hilo, kuna pia ule wasi wasi kuhusu kuzidi kwa machafuko nchini Tunisia na Algeria, ghasia za kidini nchini Misri na kile kinachoonekana kama ni matatizo katika juhudi zake za kuyafgufua mazungumzo ya amani kati ya Israel na Wapalestina.

Kuvunjika kwa serikali ya umoja wa taifa inayoongozwa na Bw Hariri nchini Lebanon kunaongeza mzigo mwengine kwa Marekani inayoangalia ushawishi wa Iran nchini humo sawa na ilivyo katika nchi jirani ya Iraq. Iran inauunga mkono muungano wa tarehe 8 Machi , unaoongozwa na kundi la Hezbollah, na ambayo kujiundoa kwake serikalini kumesababisha mgogoro huu wa sasa.

Joshua Landis anasema,kwa mara nyengine tena Lebanon inatumbukia katika janga la kuwa mhanga wa vita vya vuta nikuvute katika kanda hiyo kati ya Marekani, Israel na washirika wao kwa upande mmoja na Syria,Hezbollah na Iran ya Mahmoud Ahmadinejad upande mwengine.

Kuvunjika kwa serikali hiyo ya Lebanon hata hivyo alau kwa kipindi kifupi, hakuelekei kuirejesha tena katika machafuko sawa na yale ya Mei 2008, lakini hapana shaka yoyote kutazidisha mvutan kati ya madhebu tafauti yanayounada jamii ya nchi hiyo, ambayo katika kipindi cha utulivu cha miezi 18 iliopita ililazimika kupunguza wimbi la uwekezaji ulioinua uchumi wake.

Kwa kuwa hatua ya Hezbollah imesadifiana na mkutano kati ya Hariri na Obama Ikulu mjini Washington, inatoa ishara ya kama kwamba mlengwa zaidi alikua ni Marekani kuliko Waziri mkuu Hariri.

Msimamo wa Hezbollah

Kwa hakika chama hicho cha Washia na washirika wake wameishutumu Marekani kwa kuhujumu jitihada za pamoja za Saudi arabia na Syria, kuleta suluhisho katika mkwamo huo wa kisiasa kwa njia ya mazungumzo, jambo ambalo lilisababisaha kuvunjika kwa serikali hiyo pamoja na dhana ya kuhusishwa kwa wanaharakati kadhaa wa Hezbollah na mahakama maalum ya Umoja wa mataifa inayochunguza kuuawa kwa waziri mkuu wa zamani wa Lebanon Rafiq Hariri baba yake Saad. Kirasmi Hezbollah amehusisha na kifo cha Hariri ambaye alikua Msunni.

Majeshi ya Syria yakikondoka Lebanon mwaka 2005


Kuuawa kwake kulizusha maandamano makubwa ya upinzani wa Umma yalioongozwa navuguvugu la Machi 14 lililoongozwa na Hariri jambo ambalo lilisababisha hatimae kuondoka kwa majeshi ya Syria nchini Lebanon.

Vuguvugu hilo liliungwa mkono na utawala wa rais wa zamani wa Marekani George Bush ambaye lengo lae wakati huo lilikua ni kudhoofisha ushawishi wa Syria na mshirika wake Iran.

Utawala wa Obama umeendelea kuiunga mkono mahakama hiyo, ikiiangalia kama chombo kimoja wapo kitakachoweza kutoa nafasi ya kupatikana wizani katika nguvu za madaraka nchini Lebanon.

Hezbollah inamshikilia Saad Hariri kuikataa mahakama hiyo na kusitisha ushirikiano wa Lebanon na mahakama hiyo, jambo ambalo wachambuzi wanasema kwa Hariri itakua ni kujiuwa mwenyewe kisiasa.

Mgogoro wa awali wa kisiasa uliozuaka Mei 2008 ulipatiwa suluhisho kwa upatanishi wa Qatar na kutiwa saini makubaliano ya Doha na kuundwa serikali ya umoja wa taifa, na sasa kwa mara nyengine nchi hiyo ya ghuba imeeleza kuwa tayari kujiunga katika hatua za kuzisuluhisha tena pande zinazohusika nchini Lebanon

No comments:

Post a Comment