KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Wednesday, January 12, 2011
Maximilian Kolbe ni nani?
Maximilian Maria Kolbe (8 Januari, 1894 – 14 Agosti, 1941) alikuwa padre wa Kanisa Katoliki na mtawa wa shirika la Ndugu Wadogo Wakonventuali kutoka nchi ya Poland.
Baada ya kuanzisha chama cha Mashujaa wa Imakulata huko Roma (Italia) na Mji wa Imakulata huko Polandi, alikwenda Japani kama mmisionari.
Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia alifungwa na wafuasi wa Nazi katika kambi ya wafungwa wa siasa kule Auschwitz. Hatimaye alijitolea kushika nafasi ya mfungwa mwenzake aliyechaguliwa kuachwa bila ya chakula hadi kufa pamoja na wengine 9. Aliwaandaa hao wote kukabili kifo kwa tumaini la Kikristo na bila ya chuki, na alipobaki peke yake aliuawa kwa sindano ya sumu.
Mwaka 1982 alitangazwa na Papa Yohane Paulo II kuwa mtakatifu mfiadini. Sikukuu yake ni tarehe 14 Agosti kila mwaka
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment