KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, January 12, 2011

Matokeo kidato cha nne wasichana wang’ara


MATOKEO ya kidato cha nne yaliyotangazwa jana yanaonyesha ufaulu kwa wanafuzi wasichana umeongezeka na kufanikiwa kushika nafasi nane bora za juu.
Akitangazwa matokeo hayo, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Mitihani (Necta), Bi .Joyce Ndalichako kwa mwaka huu wasichana wameweza kufaulu na kuwapiku wavulana kwa asilimia kubwa.

Aidha alisema matokeo hayo yamedhihirisha kuwa nusus ya wanafunzi waliofanya mitihanai hiyo Oktoba mwaka jana walifeli na kupata daraja sifuri kwa mujibu wa mtokeo hayo.

Alifafanua kuwa jumla ya watahiniwa 352,840 walifanya mtihani huo na waliofaulu ni 177,021 na wengine walifeli.

Pia alisema jumla ya wanafunzi wanne walifutiwa matokeo yao kutokana na kuandika matusi kwenye karataasi zao za kuandikia majibu

No comments:

Post a Comment