KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Sunday, January 9, 2011

Mapenzi ni idadi kadhaa ya hisia zinazohusiana na mahaba Maishani



Mapenzi ni idadi kadhaa ya hisia zinazohusiana na mahaba [1] pendo na hata upendo wa Kimungu.

Neno "kupenda" linaweza kurejelea aina za hisia, hali na mitazamo tofauti, kuanzia ridhaa ya jumla ("Napenda chakula hicho"), hadi mvuto mkali kati ya watu ( "Nampenda mume wangu"). Uanuwai wa matumizi na maana, pamoja na utata wa hisia zinazohusika, hufanya kuwe na ugumu katika ufafanuzi wa dhana hii, hata ikilinganishwa na hali zingine za kihisia.

Kidhahania, mapenzi kwa kawaida yanarejelea hisia za ndani, zisizoelezeka, za kudumu kwa mtu mwingine. Hata hivyo, maelezo haya finyu pia yanashirikisha hisia tofauti, kutoka hamu na urafiki wa kimahaba na ukaribu wa kihisia wa kifamilia na kitaamuli, usiohusisha ngono [2] hadi umoja wa kina au ibada ya upendo] wa kidini. [3]

Mapenzi katika aina zake mbalimbali husimamia mafungamano kati ya binadamu na, kutokana na umuhimu wake mkuu wa kisaikolojia, ni mojawapo ya maudhui yanayopatikana sana katika sanaa

kwa habari zaidi nenda:
www.lovemaishani.blogspot.com

No comments:

Post a Comment