KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, January 10, 2011

I Coast 'yawafukuza' mabalozi wa Canada


Laurent Gbagbo


Taarifa iliyotolewa na televisheni ya taifa imesema, kiongozi aliyepo madarakani nchini Ivory Coast Laurent Gbagbo anawafukuza mabalozi wa Uingereza na Canada.

Imeelezwa kwenye taarifa hiyo kuwa hatua hiyo imechukuliwa kama mapatano. Nchi zote mbili zilisema hatua hiyo haikuwa na sababu thabiti.

Jumuiya za kimataifa zimemtambua Alassane Ouattara kama mshindi wa uchaguzi wa urais wa Novemba na kumsihi Bw Gbagbo kuachia madaraka.

Bw Ouattara ameyasihi majeshi ya Afrika Magharibi kumwondosha Bw Gbagbo.

Muungano wa kiuchumi wa nchi za Afrika Magharibi Ecowas imetishia kumtoa Bw Gbagbo kwa nguvu lakini imesema inataka kujaribu jitihada za upatanisho kwanza.

Bw Gbagbo bado anaungwa mkono na jeshi la nchi hiyo na kudhibiti vyombo vya habari vya serikali.

Uingereza na Canada ni miongoni mwa mataifa yaliyowaondosha mabalozi wao walioteuliwa na Bw Gbagbo ili kuweka wanadiplomasia waliochaguliwa na Bw Ouattara.

Mwandishi wetu wa BBC John James alisema balozi wa Uingereza, ambaye ni kama mjumbe wa nchi kadhaa eneo hilo, atakuwepo nchi jirani ya Ghana, na ubalozi wa Canada utaweza kuendelea kufanya shughuli zake kama kawaida.

No comments:

Post a Comment