KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Saturday, January 29, 2011

Mandela aruhusiwa kutoka hospitali


Bw Nelson Mandela


Aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini Nelson Mandela ametolewa hospitali ambapo alikaa kwa siku mbili.

Daktari General Vejaynand Ramlakan alisema Bw Mandela, mwenye umri wa miaka 92, ambaye alikuwa na maradhi mbalimbali yaliyo ya kawaida kwa watu wa umri yake anaendelea uzuri.

Makamu wa Rais Kgalema Motlanthe- akitumia jina lake la ukoo la Bw Mandela-alisema "Madiba anaendelea vizuri."

Siku ya Ijumaa Bw Ramlakan alisema Bw Mandela alipata matatizo ya kupumua, lakini alikuwa akiendelea vizuri na atakuwa anapata matibabu akiwa nyumbani.

Alisafiri kutoka Cape Town hadi Johannesburg siku ya Jumatano kwa kile serikali kilichoita uchunguzi wa "kitaalamu".

Hatua hiyo ilichochea wasiwasi upya juu ya afya dhaifu ya kiongozi huyo.

Marafiki na familia walimtembelea licha ya kuwepo kwa usalama wa hali ya juu siku ya Alhamis.

Afisa mwandamizi wa polisi alisema mfululizo wa magari ulikuwepo nyuma ya eneo la kuingilia katika hospitali ya Milpark mjini Johannesburg, yakijiandaa kumchukua Bw Mandela nyumbani kwake Houghton.

Shujaa huyo wa ukombozi wa Afrika Kusini-anayejulikana miongoni mwa Waafrika Kusini kwa jina lake la ukoo, Madiba- tangu ajiuzulu na masuala ya umma mwaka 2004 ameonekana kuwa dhaifu katika mara chache anazoonekana hadharani.

No comments:

Post a Comment