KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, January 29, 2011

Polisi na waandamanaji wapambana Misri

Polisi wamepambana na maelfu ya waandamanaji kwenye mji mkuu wa Misri, Cairo, baada ya sala ya Ijumaa wakitaka Rais Hosni Mubarak ajiuzulu.

Polisi walirusha mabomu ya machozi na kutumia mizinga ya maji kusambaza watu, waliokuwa wakirusha mawe.

Watu hao pia waliandamana katika miji ya Suez na Alexandria

Maandamano Misri


Serikali ilisema iko tayari kwa mjadala, lakini pia imeonya kuchukua "hatua madhubuti".

Mawasiliano ya kupata huduma za wavuti na simu za mkononi yamekatizwa.

Kulikuwa na ripoti za kuanza upya kwa mapigano, pamoja na viongozi wa upinzani kukamatwa.

Pia kulikuwa na hatua kali za kinidhamu dhidi ya kundi la kiislamu lililopogwa marufuku, the Muslim Brotherhood, baada ya kusema itaunga mkono maandamano hayo siku ya Ijumaa.

Siku ya Alhamis, mpinzani wa Misri na mshindi wa tuzo ya Nobel Mohamed ElBaradei alirejea Cairo, akiahidi naye kuandamana.

Takriban watu saba wameuawa na takriban 1,000 wamekamatwa tangu maandamanao hayo yalipoanza.

Maandamano hayo yameanza baada ya kuwepo ghasia Tunisia, yaliyosababisha kukimbia kwa Rais Zine al-Abidine Ben Ali.

No comments:

Post a Comment