KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, January 6, 2011

Kabla kura ya maoni Bashir azuru Juba


Bashir akiwa Juba


Rais wa Sudan Omar al-Bashir, yupo ziarani katika mji mkuu wa Sudan Kusini, kabla ya kuandaliwa kura ya maoni kuhusu uhuru wa Kusini, itakafanyika siku ya Jumapili ijayo.


Bwana Bashir amekutana na Rais wa eneo linalojitawala la Sudan Kusini , Salva Kiir, kujadili maswala mbali, iwapo raia wa Sudan Kusini wataamua kujitenga na Kaskazini.

Miongoni mwa masuala hayo ni pamoja na usimamizi wa raslimali za maji na mafuta na mustakabal wa raia wa kusini wanaoishi kaskazini.

Rais Omar al-Bashir amesema atasikitishwa sana kuona Sudan itagawanyika na kuwa nchi mbili.

Aliyasema hayo katika mji wa Juba, mji mkuu wa Sudan Kusini, wakati akihutubia moja kwa moja kupitia televisheni.

Hata hivyo Bw Bashir amesema atafurahi iwapo kuundwa kwa nchi hizo mbili na kuwa mataifa mawili, kutaleta kile alichokiita, amani ya kweli kwa pande zote mbili za Sudan.

Ameongeza ataheshimu matakwa ya watu na ataunga mkono maendeleo ya Sudan Kusini iwapo wataamua kujitawala wenyewe

No comments:

Post a Comment