KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, January 6, 2011

Buhari ateuliwa kugombea urais Nigeria

Mohammadu Buhari

Nchini Nigeria chama kipya cha upinzani, Congress for Political Change, kimemteu mtawala wa zamani wa kijeshi, Muhammadu Buhari, kugombea Urais kwa tiketi ya chama hicho katika uchaguzi utakaofanyika mwezi Aprili.
Bw Buhari aliitawala Nigeria kwa kipindi cha miezi ishirini, miaka ya themanini na anafahamika sana kwa sheria zake kali za kuwaadhibu watu.

Waandishi wa habari wamesema chama hicho kinatarajiwa kufanya vizuri katika uchaguzi huo, kaskazini mwa Nigeria ambako Bw Buhari anatoka na huenda akawa mgombea mkuu wa upinzani ikiwa Rais Goodlack Jonathan atateuliwa kugombea kiti hicho kwa chama tawala cha PDP kama inavyotarajiwa

No comments:

Post a Comment