KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, January 6, 2011

Bei ya chakula yapanda duniani


Chakula kilipanda sana mwezi uliopita


Takwimu mpya za Umoja wa Mataifa, zimeonyesha bei ya vyakula ikipanda kwa kiwango cha juu zaidi mwezi jana.




Idara ya Umoja wa Mataifa inayotathmini bei ya chakula, imesema vyakula vilivyopanda bei ni pamoja na sukari, mafuta ya kupikia, nyama na nafaka.

Mara ya mwisho bei ya chakula kupanda ilikuwa mwaka 2008 hali iliyochochea maandamano makubwa katika baadhi ya nchi.

Wakati huo huo baraza kuu la nishati duniani, limeonya kurejea kwa msukosuko wa kifedha kama ulivyoshuhudiwa mwaka 2008 kutokana na gharama ya juu ya mafuta.

Mkuu wa IEA ameambia BBC, malighafi ya mafuta inauzwa dola 90 kwa pipa. Amesema hali hii ni ishara ya hali mwaka 2008

No comments:

Post a Comment