KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, January 6, 2011

AU kutoafiki I.Coast mgawo wa madaraka


Mpatanishi mkuu wa Muungano wa Africa- AU, katika mzozo wa kisiasa wa Ivory Coast, ambaye pia ni Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga, amesema AU haiwezi kukubali mfumo wa kugawana madaraka, ili kutatua mzozo wa kisiasa nchini Ivory Coast.

Akizungumza katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta, mjini Nairobi, muda mfupi baada ya kurejea kutoka Ivory Coast, Bw Odinga alisema jopo lililoteuliwa na AU na Jumuia ya Kiuchumi ya mataifa ya Afrika Magharibi- ECOWAS, limefanikiwa kumshawishi Rais Luarent Gbagbo, kuanzisha mazungumzo ya kumkabidhi mpinzani wake, Oullussanne Outtarra madaraka.


Odinga amesema tayari Bw Gbagbo amewaondoa wanajeshi waliokuwa wamezingira makao makuu ya Bw Outtarra, katika juhudi za kutekeleza maazimio yaliyoafikiwa.

Hata hivyo amesema ECOWAS na AU haviwezi kukubali Bw Gbago kuendelea kubakia madaraka, endapo mazungumzo hayo yatashindikana.

No comments:

Post a Comment