KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, December 11, 2010

Zitto Kabwe Atishiwa Kuuliwa


KADRI siku zinavyozidi kusogea mbunge wa Kigoma Kaskazini [CHADEMA] Zitto Kabwe yuko kwenye wimbi la wasiwasi wa kuuliwa kutokana na kupata ujumbe mfupi wa maneno wa simu ulioashiria kutishiwa uhai wake.
Ujumbe huo ambao unaleta minong’ono ya hapa na pale wka wadau wa siasa nchini kutokana na kutishiwa maisha kiongozi huyo wa juu katika medali za siasa.

Kufuatia hali hiyo chama cha Maendeleo na Demokrasia [CHADEMA] kimekuwa na migawanyiko ya hapa na pale kupelekea kutopatikana kwa maelewano ndani ya chama hicho.

Imedaiwa kuwa, baadhi ya viongozi wa chama hicho wanaandaa mkakati wa kummaliza Zitto ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho kwa kile kinachodaiwa ni kukisaliti chama.

Awali kabla ya migogoro ndani ya chamda hicho, Wabunge wa CHADEMA walitia mgomo bungeni na kutoka nje ya ukumbi wa bunge kwa kudai kuwa hawamtambui Rais Jakaya Kikwete na kususia hotuba zake na badhi ya shughuli za serikali hiyo.

Hali hiyo ilikuwa tofauti kwa upande wa Zitto kwani yeye hakushiriki katika mgomo huo na huo ndio ulikuwa mwanzo wa migogoro ndani ya chama hicho.

Nae Mbunge wwa Ubunge nae hakuwepo katika mgomo huo kwani yeye hakufika kabisa ndani ya ukumbi huo kwa madai alikuwa mgonjwa na hakuweza kufika bungeni kwa siku hiyo.

Hata hivyo Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Robert Manumba, alimtaka Zitto kufata taratibu za kipolisi kuripoti tukio hilo katika kituo chochote cha polisi kwani hawataweza kulizungumzia suala hilo moja kwa moja hadi utaratibu huo ufuatwe

No comments:

Post a Comment