KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, December 11, 2010

'Vibaraka wa CCM ndani ya CHADEMA'


SIKU chache baada ya kuzuka hali ya kutofautiana kimsimamo kulikotokana na suala la kususia hotuba ya Rais Jakaya Kikwete bungeni, hali imeanza kuwa tete ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo,CHADEMA.
Habari za uhakika kutoka chanzo chetu cha habari zinasema kuwa, uongozi wa Chandema umebaini kuwapo kwa 'Mamluki' wa CCM ndani ya chama hicho ambao wametumwa kazi ya kukisambaratisha mapema kabla ya chaguzi zijazo,ukiwemo ule wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Imeelezwa kuwa, uongozi wa ngazi ya juu umebaini hali hiyo ya kuwapo kwa mamluki mara baada ya kumalizika kwa kikao kilichopita cha bunge la Jamhuri ya Muungano, na kati ya mamluki hao ni waheshimiwa wabunge waliopita kwa tiketi ya chama hicho.

Chanzo hicho kilieleza kuwa, mamluki hao wamejipenyeza katika ngazi ya wilaya, mkoa mpaka taifa na wanashirikiana na madiwani na wabunge wa chama hicho na kazi iliyopo mbele yao ni kuisambaratisha Chadema katika ngazi husika.

Taarifa za kuwepo kwa mamluki wa kukivuruga chama hicho zimeanza kufanyiwa kazi na uongozi wa ngazi za juu ambapo habari tulizonazo ni kwamba baadhi ya wabunge na madiwani wameanza kufuatiliwa kwa karibu na baadhi yao wameshaanza kuwekwa kiti moto.

Imebainishwa kuwa, karibu katika kila kata na jimbo ambalo Chadema wameshinda CCM imeingiza mamluki wa kuhakikisha wanabuni mikakati ya kukidhohofisha chama na kisha wahusika wa ngazi hiyo waonekane hawafai na kutumiliwa.

Mbunge mmoja wa Chadema ambaye hata hivyo hakutaka jina lake litajwe alisema kuwa uongozi wa Chadema umepewa majina ya madiwani na wabunge wanaosaidiana na mamluki waliopewa kazi ya kukisambaratisha chama kupitia migorogoro ya ndani ya chama.

"Majina ya mamluki wote yapo kwa uongozi ni juu yao sasa kuanza kuyafanyia kazi na wameahidi kuwakabili kupitia vikao vya ndani vya chama, ila ukweli wa mambo upo hivi".

"Ni mtihani mkubwa kwa uongozi kwani baadhi yao ni wana majina maarufu na wazoefu wa siasa za upinzani, ila wapo pale kwa ajili ya kukisaidia Chama Cha Mapinduzi kuvunja nguvu ya Chadema na kuisafisha njia CCM kuelekea chaguzi zijazo" alizungumza mbunge huyo kwa uhakika wa hicho anachokielezea.

Hata hivyo Richard Tambwe Hiza ambaye ni mmoja wa wenye dhamana ya kitengo cha Propaganda na Uenezi, CCM taifa alizungumzia taarifa hizi na kusema shutuma hizo ni moja ya staili ya vyama vyote vya upinzani nchini ambapo kila panapotokea migogoro ya ndani kwa ndani baina yao mwisho wa yote ukihusisha Chama Cha Mapinduzi ndicho kinachowasababishia migogogoro na mivutano yao

No comments:

Post a Comment