KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, December 30, 2010

Waandamanaji Misri watafuta suluhu mpya


Misri


Waandamanaji katika eneo la wazi mjini Cairo, Tahrir wametoa wito upya wa kumtoa Rais wa Misri Hosni Mubarak, katika kipindi cha wiki mbili cha kampeni zao.

Maelfu ya watu bado wamehodhi uwanja huo lakini wamesogezwa nyuma na wanajeshi, wakijitahidi kuweka nafasi ili magari yaweze kupita.

Mazungumzo yamefanikiwa kwa kiasi kidogo na uwezekano wa Bw Mubarak kujiuzulu ni mdogo sana.

Serikali ya nchi hiyo imetangaza tahafifu, ikiwemo ongezeko la asilimia 15 kwa mishahara ya wafanyakazi milioni sita wa sekta za umma.

Mwandishi wa BBC Jon Leyne, mjini Cairo, alisema hiyo ni ishara kuwa serikali inajaribu kuimarisha nguvu zake.

Rais wa Marekani Barack Obama amepunguza makali ya ukosoaji wake, na kuzungumzia uzuri wa kuwepo na majadiliano.

Bw Obama alisema Washington, " Bila shaka, Misri lazima ifanye majadiliano, na nadhani yanaenda uzuri."

No comments:

Post a Comment