KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, December 14, 2010

Vikwazo zaidi vya kiuchumi na kisiasa vinazidi kutolewa dhidi ya Laurent Gbagbo

Balozi wa Umoja wa mataifa nchini Ivory Coast Guy-Alain Emanuel Gauze, kushoto.

Rais wa Ivory Coast ambaye amekataa kuondoka madarakani baada ya uchaguzi wa mwezi uliopita.

Baraza kuu la umoja wa mataifa sasa limemtambua rasmi mpinzani wa bwana Gbagbo, Alassane Ouattara, kuwa ndiye rais wa haki wa taifa la Ivory Coast.

Na benki kuu ya muungano wa kiuchumi na kifedha kwa mataifa ya kanda ya Afrika ya magaribi pia imemtambua Allasane Ouattara kuwa ndiye rais wa taifa hilo.

Laurent Gbagbo

Benki hiyo imesema itazuia utoaji wa pesa kwa serikali ya bwana Gbagbo. Awali baraza la umoja wa mataifa kuhusu haki za kibinadamu lilileezea wasiwasi mkubwa kuhusiana na machafuko yaliyozuka nchini Ivory Coast baada ya uchaguzi huo.

Katika kikao maalum mjini Geneva , baraza hilo liliidhinisha kwa kauli azimio la kulaani vikali kile wanachama walikitaja kuwa uhalifu na kumuru kurejelewa kwa utawala wa sheria nchini humo.

Afisa wa ngazi ya juu katika umoja wa mataifa amesema uchunguzi umebaini kuwa zaidi ya watu mia moja sabini wameuwawa tisaini wameteswa na zaidi ya mia tano kukamatwa

No comments:

Post a Comment