KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, December 14, 2010

Tanesco yatangaza mgawo mpya utakaodumu mwezi mmoja



SHIRIKA la Umeme Tanzania [Tanesco] jana limetangaza mgao mpya wan chi nzima utakaodumu kwa kipindi cha mwezi mmoja mbali na ule uliotangazwa awali.
Tangazo hilo lilitolewa jana na Afisa Uhusiano wa Shirika hilo Bi. Badra Masoud na kusema mgao huo utahusika nchi nzima kutokana na sababu ambazo ziko nje ya shirika hilo.

Badra alisema kuwa mgao huo utasababishwa utengenezwaji wa kisima cha kampuni ya Pan African Energy inayozalisha gesi eneo la Songo Songo.

Kisima hicho am bacho huzaisha gesi hiyo na kusafirisha katika kampun ya Songas ambko huzalisha megawati 180 na baadae kuiuzia shirika hilo eneo la Ubungo.

Hivyo kutokana na sababu hiyo ya kukifanyia matengenezo kisima hicho kimoja kati ya vitano vya kampuni hiyo itasababihsa upungufu wa megawati 40 na kulazimika kufnya mgao huo kutokana na upungufu huo.

Alieleza kuwa mgawo huo utaanzia majira ya saa 2 asubuhi hadi saa 12 jioni katika baadhi ya maeneo, na maeneo mengine yaliyokosa umeme kwa muda huo wataanza kupata umeme kuanzia saa 12 jioni hadi saa 5 usiku ambapo ratiba hiyo ni mara tatu kwa wiki.

Hata hivyo alisema ratiba kamili juu ya ratiba hiyo itatolewa katika vyombo vya habari na wananchi waangalie ratiba hizo kupitia vyombo hivyo.

Aidha alisema maeneo ya viwanda, hospitali, pampu za maji, migodi havitaathirika sana na watakatiwa umeme usiku na mchana kutwa kuwachia ili waweze kuzalisha.

“ Ila katika kipindi cha sikuuu tutahakikisha umeme utakuwepo ili wananchi waweze kusherehekea sikukuu vizuri bila kero ya kukosa umeme” alsiema Badra

No comments:

Post a Comment