KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, December 30, 2010

Utawala mpya wa kijeshi nchini Misri umesema unalifunga bunge la kuisimamisha katika ya nchi kwa muda.


Waandamanaji mjini Cairo


Katika taarifa kupitia televsheni ya taifa, baraza la juu la kijeshi limesema litakaa madarakani kwa miezi sita, au mpaka wakati utakapofanyika uchaguzi.

Bunge la sasa la Misri, limetawaliwa na wafuasi wa Rais Hosni Mubarak, ambaye aliondoka madarakani siku ya Ijumaa, kufuatia siku 18 za maandamano.


Waandamanaji katika eneo la wazi la Tahrir


Mapema kulikuwa na mzozano katika eneo la wazi la Tahrir, baada ya waandamanaji kugomea hatua za jeshi za kuwaondoa katika eneo hilo.

Polisi wa kijeshi wametaka mahema kuondolewa katika eneo hilo ambalo ni kitovu cha maandamano yaliyosababisha kuondoka kwa Bw Mubarak.

Mwandishi wa BBC Wyre Davis aliyeko mjini Cairo anasema hali katika eneo hilo la wazi imekuwa kama mvutano wa kirafiki, lakini wandamanaji wamesema wataendelea kusalia hapo hapo


Polisi wa kijeshi wakiwa na waandamanaji


Taarifa ya jeshi ilioyosomwa kupitia televisheni ya taifa siku ya Jumapili imesema itasitisha katiba iliyopo na kuunda kamati itakayoandika muswada mpya wa katiba, kabla ya kufanyika kwa kura ya maoni.

Katiba ya sasa inazuia vyama ving vya kisiasa na makundi kushiriki katika uchaguzi, na hivyo kufanya bunge la nchi hiyo kujaa wafuasi wa chama cha National Democratic, ambacho kinamtii Bw Mubarak.

Mwandishi wetu anasema, tangazo hili jipya linamaanisha uchaguziutafanyika mwezi Julai au Agosti, badala ya Septemba kama ilivyokuwa imepangwa.

No comments:

Post a Comment