KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, December 15, 2010

UN yajibu vitisho vya Gbagbo

Laurent Gbago-amekwamilia madaraka Ivory Coast

Laurent Gbago-amekwamilia madaraka Ivory Coast.
Umoja wa mataifa umejibu vikali hatua ya kuwafukuza wanajeshi wa umoja wa mataifa nchini Ivory Coast huku mzozo kuhusu uchaguzi wa urais wa mwezi uliopita ukizidi kutokota
Wanajeshi wa UN Ivory Coast

Laurent Gbagbo --ambaye amekataa kuondoka madarakani baada ya kushindwa katika uchaguzi huo anasema majeshi ya ufaransa na yale ya umoja wa mataifa ni sharti yaondoke nchini kwa kuwa yanashirikiana na wapinzani wake.

Lakini katibu mkuu wa umoja wa mataifa, Ban Ki Moon, amesisitiza kuwa majeshi ya umoja wa mataifa hayataondoka nchini humo hadi pale yatakapokamilisha mhula wake wa kuhudumu mwishoni mwa mwezi huu.

Bwana Ban ki Moon ameonya kuchukuwa hatua kali iwapo wanajeshi wa kulinda amani wa umoja wa mataifa watashambuliwa na wanajeshi walio watiifu kwa bwana Gbagbo.

Hapo awali umoja huo ulitangaza kuwa wanajeshi wake wana idhini ya kujimbu mashambulizi iwapo itawabidi.

Jamii ya kimataifa inamtambua mpinzani wa bwana Gbagbo, Alassane Outtara kuwa ndiye aliyeshinda uchaguzi huo.

No comments:

Post a Comment