KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, December 15, 2010

Bashir asalimu amri kuhusu kura ya maoni


Mwanamke akicharazwa viboko.

Sheria za kiislamu zitakuwa kali Kaskazini.
Rais wa marekani Barrack Obama ametangaza kuwa swala la Sudan ni mojawepo wa ajenda kubwa ya mashauri ya nchi za kigeni ya serikali yake.

Rais Omar Bashir.

Msemaji wa Ikulu ya White House Mike Hammer amesema bwana Obama amekwishawaandikia barua viongozi wa Afrika akiwataka kuunga mkono kura ya maoni kuhusu uhuru wa Sudan Kusini itakayoandaliwa kwa njia ya amani.

Awali rais wa Sudan, Omar al-Bashir, alisema Sudan Kaskazini itaimarisha sheria za kiislamu ikiwa Sudan kusini itapiga kura ya kujipatia uhuru.


Bwana Bashir amesema kwamba ikiwa taifa hilo litagawanywa, katiba ya Sudan itabadilishwa , Kiarabu itakuwa ndiyo lugha ya pekee, dini ya pekee itakuwa ni Uislamu, na sharia ndiyo katiba ya pekee itakayotumika nchini humo.

Mwandishi wa BBC mjini Khartoum amesema maneno ya bwana Bashir yanawatia hofu raia wa Sudan Kusini ambao si waislamu na ambao wanaishi Kaskazini.

Katika mkataba wa amani wa mwaka 2005 uliomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe, raia wa Sudan Kusini walilindwa dhidi ya makali ya sharia.

No comments:

Post a Comment