KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Thursday, December 2, 2010
Umeme tatizo Dar wengi walalamikia uchumi
JIJI la Dar es Salaam na vitongoji vyake limekuwa na tatizo la kukosa umeme w uhakika ni zaidi ya wiki mbili sasa baada ya shirika la umeme nchini kutangaza mgawo wa umeme huo.
Kutokana na ukosefu wa umeme huo, wakazis wengi wa jiji wamekuwa wakilalamikia mgao huo kwa kuwa ulikuwa ukirudisha maendeleo nyuma kutokana na ukosefu wa umeme wa uhakika.
Hivyo kufuatia hali hiyo wakazi hao wamekuwa wakiiomba shirika hilo kushughulikia tatizo hilo kwa haraka kwa kuwa wamekuwa wakipoteza dira katika kipato chao cha kila siku.
"Kwa kweli tunasikitika sana, mana wengine hatufanyi kazi maofisini useme mwisho wa mwezi nitapokea mshahara kama kawaida, sisi tunategemea huo umeme ndio tuingize kipato chetu cha kila siku kutokana na shughuli zetu tunazozifanya" walilalama baadhi ya wafanyabiashara wa maeneo ya kati kati ya jiji
Tatizo hilo la kukosa umeme limetokanakwa kuharibika kwa mitambo mbalimbali na ukosefu wa vyanzo vya kuzalish umeme huo kutokana na kukosa maji katika vyanzo hivyo na mabadiliko ya hali ya hewa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment