KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, December 14, 2010

Rais Jonathan aahidi kuwakamata walipuaji

Rais wa Nigeria amesema serikali yake itafanya kila iwezalo kuwatafuta waliohusika na mfululizo wa mashambulio ya mabomu yaliyosababisha vifo vya watu wasiopungua 32 karibu na mji wa Jos.

Ahadi....Goodluck Jonathan


Rais Goodluck Jonathan ameahidi kuwa waliopanga mashambulio hayo "watakabiliana na sheria". Hakuna kundi ambalo limesema limehusika na mashambulio hayo.

Mashambulio hayo yaliyotokea siku ya kuamkia Krismasi, yamefanyika katika eneo ambalo karibu watu 1,00 waliuawa katika mapigano ya kidini mwaka huu.


Jos


Mapigano ya siku zilizopita yamekuwa kati ya magenge ya Waisilam na Wakristo, lakini wachambuzi wanasema sababu hasa za ghasia ni za kiuchumi zaidi kuliko kidini.

Waisilam kwa kawaida hutokea jamii inayozungumza lugha ya Hausa, au Fulani. Mara nyingi huwa watu wa kuhama hama na huendesha maisha yao kwa ufugaji au biashara ndogondogo.

Wakristo kutoka jamii ya Berom, Anaguta na Afisare kijadi ni wakulima.


Ghasia zilizotokea Jos


Baadhi ya Wakristo wakulima, wanahisi wanatishwa na Waisilam wanaozungumza kihausa wanaokuja kutoka kaskazini wakitafuta malisho ya mifugo yao.

Huko Maiduguri, watu wanaoshukiwa kuwa wafuasi wa kundi la Waisilam wenye itikadi kali, walishambulia makanisa mawili siku ya Ijumaa.

Shirika la habari la Reuters limeripoti kuwa katika tukio moja, bomu la petroli liliua watu watano, akiwemo padre wa Kibatisti

No comments:

Post a Comment