KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, December 2, 2010

Profesa: Maji ya chupa siyo salama kwa kunywa


Fredy Azzah
MAJI ya kunywa yanayouzwa kwenye chupa, yameelezwa kutokuwa salama sana kwa afya za watumiaji kutokana na wafanyabiashara wengi wa bidhaa hiyo, kujali zaidi maslai yao badala ya kuangalia ubora wa bidhaa.

Hayo yalibainishwa jana jijini Dar es Salaam na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria, Taaluma Profesa Elifas Bisanda, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hotuba inayotarajiwa kutolewa ijumaa wiki hii na Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Tolly Mbwete.
Kwa mujibu wa Profesa Bisanda, hatuba hiyo ambayo kitaalamu hujulikana ‘Professorial Inaugural Lecture’, ni matokeo ya utafiti uliofanywa na Profesa Mbwete, ambaye kitaaluma ni mtaalam wa nishati ya maji.

“Kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hii ni mara ya kwanza kufanya tukio kama hili, ingawa profesa Mbwete alishatoa tena hotuba kama hii alipokuwa chuo kikuu cha Dar es Salaam, hotuba hiyo ilihusu njia rahisi ya kuchuja maji kwa kutumia mchanga.

“Hotuba ya safari hii ambayo ipo kwenye kitabu chenye takribani kurasa 100, imeangalia zaidi maji ya kunywa yanayouzwa kwenye chupa, kwa kiasi kikubwa amebaini kuwa maji, siyo salama sana na kuna mapendekezo kadhaa yaliyotolewa ili kunusuru afya za Watanzania.”
Athari zaidi za maji hayo, zinatarajiwa kutolewa siku ijumaa wakati Profesa Mbwete akiwasilisha hotuba yake.

Profesa Bisanda alisema baadhi ya mapendekezo hayo ni pamoja na vyombo vinavyohusika na huduma ya maji safi, kuongezewa uwezo ili kuzalisha maji safi na salama na wananchi wataweza kuyanywa moja kwa moja yakitoka bombani.

Pia serikali imetakiwa kuondoa urasimu katika sekta ya kuzalisha na kusambazamaji safi ili kuchochea uwekezaji katika sekta hiyo ili huduma hiyo iweze kutolewa kwa viwango vyenye ubora.

“Kwa sasa kunaongezeko kubwa la wafanyabiasha wa maji haya, (Shirika la Viwango) TBS wanapelekewa sampuli ya maji mara ya kwanza tu, kabla hawajatoa kibali, kikishatolewa wanaendelea kuzalisha bila kuchunguzwa ubora wa maji hayo,” alisema Profesa.

Kila baada ya miaka mitatu baada ya Profesa msaidizi kuwa Profesa kamili, hupaswa kutoa hutoba inayohusu mada aliyoifanyia uchungizi wa kina ili kuisaidia jamii

No comments:

Post a Comment