KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Thursday, December 2, 2010

Pombe za sherehe zamuabisha, akimbiwa na mpenzi wake


ULE USEMI unaosema pombe si chai na watu wengine wakaupuuza usemi huo na baadhi yao huadhirika mbele ya macho ya watu kwa kukaidi usemi huo.
Jana mwanaume aliyetambuika kwa jina Mr. Mtweve alijikuta akimuacha solemba mwanamke mmoja aliyekuja nae kwenye sherehe ya kuwapongeza maharusi iliyofanyika maeneo ya Msasani baada ya dada huyo kulewa na kuzidiwa na pombe na kuanza kufanya vituko visivyostahili mbele ya macho ya watu.

Mtweve alimkana mwanamke huyo baada ya kumdhalilisha mbele ya marafiki na jamaa kwa kuwa aliona angeweza kupata aibu ambayo ingeweza kumvunjia ndoa yake.

Mwanadada huyo mrembo alitinga na jamaa yake huyo ukumbini hapo majira ya saa 12 jioni akiwa amevalia vazi moja machachari linaloonyesha baadhi viungo mwilini mwake na kuonekana kuwa kivutio kwa wale ambao hupenda wanawake wanaovaa nusu uchi.

Dada huyo alionekana kuzimiliki vyema pombe aina ya Ndovu na kwa mujibu wa muhudumu aliyekuwa akihudumia meza hiyo ukumbini hapo alidai kuwa hadi majira ya saa 3 usiku dada huyo alishaweza kunywa chupa zipatazo nane na kadri muda ulivyozidi kwenda dada huyo alizidi kuagizia kinywaji hicho.

Hali ilianza kubadilika baada ya wageni waalikwa kutakiwa kutoa zawadi walizonazo kuwapongeza maharudi hao, dada huyo alianza kuonyesha vituko hali iliyofanya kila mmoja kumshangaa ukumbini humo.

Dada huyo kila baada ya sekunde huinuka kitini na kwenda kumpiga busu matata bwana harusi hali hiyo ilipojitokeza mara kwa mara kila mmoja alianza kuhoji ni kwa nini hali hiyo ilikuwa ikijitokeza.

Mbali na hilo dada huyo alionekana akicheza huku akifunua nguo hali iliyofanya marafiki wa mpenzi wake wamtulize na kumrudisha kitini kwa kuwa waligundua alikuwa amezidiwa na pombe.

Dada huyo alizidi kufanya vituko ukumbini hapo hali iliyofanya Mr. Mtweve atoke nje na kuwasha gari na kuondoka na kumuacha mwanamke huyo ukumbini humo bila ya kuwaaga marafiki zake.

Wakati sherehe hiyo ilipokuwa ikikaribia kuisha kila mmoja alikuwa akitoka na mwenzi wake na hali ilikuwa ngumu kwa dada huyo baada ya kutokumuona jamaa yake huyo na kuanza kuvamia hovyo na kuomba msaada afikishwe nyumbani kwake.

Hata hivyo msaada huo alikuwa akiomba zaidi kwa wanaume na walishindwa kumsaidia kwa kuwa kila mmoja alikuwa na mkewe aliyekuja nae mahali hapo.

Hata hivyo Nifahamishe.com ilijaribu kufanya mazungumzo mafupi na mmoja wa marafiki wa Mr. Mtweve na kuthibitishiwa kuwa ni kweli dada huyo alikuja na rafiki yao huyo lakini alimuacha kwa kuogopa fedhaha na aibu na kuogopa kuvunja ndoa yake kwani alikuja na dada huyo akimuacha mkewe nyumbani kwa kujua huenda angekuwa mstaarabu.

Alidai kuwa rafiki yao alimuacha mke wake nyumbani kwa kuwa alkuwa na mtoto mdogo ametoka kujifungua hivi karibuni

No comments:

Post a Comment