KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, December 30, 2010

Polisi sanamu




Sanamu moja lililovalishwa nguo za kipolisi na kofia yake, na kuwekwa katika kibanda cha vioo cha polisi, limezua sokomoko nchini Uchina. Kwa mujibu wa mtandao wa Guangzhou Daily, tukio hilo limetokea katika jiji la Putia, katika jimbo la Fujian mashariki mwa Uchina. Guangzhou imechapisha picha ya sanamu hilo likiwa ndani ya moja ya vibanda vinavyotumiwa na polisi kwa ajili ya kuweka ulinzi katika maeneo mbalimbali jijini humo.

Picha hiyo imeonesha polisi huyo mwanasesere akiwa peke yake ndani ya kibanda hicho. Utafiti zaidi wa vyombo vya habari nchini humo viligundua baadaye kuwa, sanamu hilo liliwekwa hapo kuchukua zamu ya ulinzi, kutokana na ukosefu wa polisi wa kutosha jijini humo.


Sanamu hilo hata hivyo liliondolewa baada ya kumaliza zamu yake ya ulinzi. Maoni mbalimbali yametoklewa kuhusiana na tukio hilo, wengine wakisema ni ubunifu wa aina yake, huku wengine wakishutumu na kusema wanawalaghai watu kuhusu usalama wao

No comments:

Post a Comment