KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, December 30, 2010

Ofisa Tanesco mbaroni Kwa Wizi wa Tsh. Bilioni Moja



JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limemtia mbaroni ofisa wa shirika la umeme Tanzania [Tanesco] kwa tuhuma za kuliibia shirika hilo zaidi ya Shilingi bilioni moja.
Imedaiwa kuwa kuwa afisa huyo amejizolea zaidi ya bilion 1.3 na kuliingiza hasara shirika hilo na kushuka kwa mapato kutokana na fedha hizo.

Taarifa hiyo ilisema kuwa fedha hizo zilizoibwa zilitokana na mauzo ya umeme wa Luku na kudaiwa aliiba umeme huo kwa kushirikiana na wafanyabiashara mbalimbali waliojuwa wakinunua umeme katika kituo hicho.

Afisa huyo ambaye ni Mhasibu Mwandamizi wa Mapato jina linahifadhiwa kutokanda na sababu za kipolisi alilidaiwa kuiba fedha hizo kati ya Oktoba 2009 hadi 2010 katika ofisi ya tanesco mkoa wa Kinondoni.

Hasara hiyo iligundulika kuunda timu kukagua mapato ya ndani ya ndipo ilipobainika kuwa kuna hasara ya fedha hizo na kubainika kuwa afisa huyo alikuwa na hatia na hatua iliyochukuliwa ni kukatisha mkataba wake wa ajira.

“Na wakaguzi wakaamua kumfikisha polisi kituo kikuu kwa hatua zaidi za kishea” alisema Mhando mkurugenzi wa shirika hilo.

Tanesco hivi sasa wanakabiliwa deni la kuilipa fidia ya shilingi bilioni 94 kampuni ya kufua umeme ya Dowans hatua iliyochukuliwa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Kibiashara (ICC).

No comments:

Post a Comment