KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, December 30, 2010

CUF yaandaa maandamano kupinga malipo Dowans


CHAMA Cha Wananchi [CUF], kinatarajia kuongoza maandamano ya amani kupinga serikali kuilipa mabilioni ya shilingi Kampuni hewa ya kufua umeme ya Dowans.
Hayo yalijulikana jana wakati Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Bw. Mtatiro Julius alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Alisema kuwa maandamano hayo yanatarajiwa kufanyika Februari 7 mwaka huu kupinga serikali isilipe fedha hizo kwa kampuni hiyo.

Alisema maandamdano hayo yataanzia eneo la Buguruni Malapa na kuishia katika viwanja vya Kidongechekundu.

Alisema maandamano hayo yataongozwa na mwenyekiti wa chama hicho Profesa Ibrahim Lipumba wakiwemo na viongozi wa juu wa chama hicho.

Mtatiro aliwafafanulia waansihi wa habri kuwa, chamda hicho kimekwisha litaarifu Jeshi la Polisi kupitia barua yenye kumbukumbu namba CUF/AK/DSM/NKM/B/002/A2/2011/08 ya Januari 28 , 2011.

Mtatiro alidai endapo serikali italipa fedha hizo wananchi wataathirika kwa kiasi kikubwa kutokana na malipo ya mabilioni ya shilingi

Alisema kwa Chama cha Mapinduzi kimekuwa ikiwakandamiza wananchi siku hadi siku na hawaoni sababu ya kulipa kampuni hiyo hewa iliyozasliwa kutokana na Richmond na hadi sasa Dowans sakata ambalo linaumiza vichwa watanzania kwakuwa haijafahamika nani mmiliki wa kampuni hiyo

No comments:

Post a Comment