KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Wednesday, December 15, 2010

Noti mpya kuanza kutumika Januari Mosi 2011


BENKI KUU ya Tanzania (BOT), imetoa noti mpya zenye sura tofauti ambazo zitaanza kutumika mwanzoni mwa 2011 nchini kote.


Hayo yalisemwa jijini Dare s Salaam na Gavana wa Benki hiyo, Profesa Benno Ndulu, wakati wa uzinduzi wa noti hizo.

Alisema noti hizo zitaanza kutumika mwanzoni mwa mwa mwaka 2011 Januari Mosi na kusema zimetengenezwa katika umakini mkubwa ambazo zitakidhi matakwa ya watanzania.

Aidha aliwataka watanzania kutambua kuwa noti za zamani zitatumika kama kawaida hadi hapo zitakapoisha mikononi mwa watanzania na kutoleta ukorofi katika noti hizo.

Alisema noti hizo zimetolewa katika ubora na kuzuia ufujaji uliokuwa ukifanywa awali katika noti hizo na zina uwezo wa kudumu muda mrefu.

Pia noti hizo zimebadilishwa ukubwa wa noti na kuwa ndogo na hali hiyo imesema “ noti hizi zitaweza kuhifadhiwa vizuri katika waleti za watanzania na kuondoa usumbufu wa upana kama ilivyokuwa awali” alisema Ndulu

No comments:

Post a Comment