KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Thursday, December 30, 2010
Mazishi ya Shoga wa Uganda Yazua Balaa
Mazishi ya shoga wa nchini Uganda David Kato ambaye alikuwa mwanaharakati wa kutetea haki za mashoga wenzake nchini humo, yalikumbwa na balaa baada ya mchungaji kuwaambia waombelezaji wa msiba kuwa ushoga ni dhambi na wanaume waache kujigeuza wanawak
Hasira zilitanda miongoni mwa mashoga na wasagaji wa nchini Uganda ambao walihudhuria mazishi ya David Kato, shoga mwanaharakati wa kutetea haki za mashoga nchini Uganda ambaye aliuliwa nyumbani kwa kushushiwa kipigo cha nguvu na watu wasiojulikana.
Wakati misa ya mazishi ikiendelea, mchungaji aliyekuwa akiendesha misa hiyo aliwageukia waombelezaji na kuwaambia kuwa ushoga na usagaji ni dhambi na hivyo watu wanaofanya vitendo hivyo watubu na kumrudia Mungu au la watakumbana na adhabu kali za Mungu.
Mchungaji Thomas Musoke akimalizia misa ya David Kato aliyeuliwa siku ya jumatano nyumbani kwake kwa kusema "Dunia inaelekea kubaya, watu wanayapa mgongo maandiko, wanalazimika kuacha mchezo wanaoufanya na kumrudia Mungu, huwezi kumtamani mwanaume mwenzako".
Ghafla mmoja wa mashoga alinyanyuka na kumfokea Mchungaji Musoke, "Hatujaja hapa kupigana", alisema huku mwanamke mmoja msagaji akiibuka na kusema "Wewe sio mtu wa kutujaji sisi, Kato ameenda kwa Mungu wake aliyemuumba Sisi ni nani mpaka tumhukumu Kato?".
Mchungaji Musoke alinyang'anywa mikrofoni na kuanza kusukumwa sukumwa na kuwafanya polisi waliokuwepo kwenye mazishi hayo waingilie kati na kumuondosha eneo hilo.
Kifo cha Kato kimekuwa gumzo kwenye vyombo vya habari vya magharibi ambapo taasisi za kutetea mashoga na wasagaji zimekuwa zikilaani kuuliwa kwake. Hata hivyo nchini Uganda habari za kuuliwa kwake hazijapewa kipaumbele.
Kato alikutwa ameuliwa ndani ya nyumba yake mjini Kampala baada ya kushushiwa kipigo cha nguvu na watu wasiojulikana.
Kato alijipatia umaarufu nchini Uganda baada ya kulifikisha mahakamani gazeti la Rolling Stone kwa kuitoa picha yake kwenye gazeti na kumtangaza kuwa ni shoga.
Taarifa za awali zimesema kwamba watu ambao hawajajulikana walivamia nyumba yake na kumshushia kipigo kizito kilichopelekea kufariki kwake.
Polisi wamemkamata mshukiwa mmoja. Hata hivyo mshukiwa mkuu ambaye alikuwa ni mwanaume aliyekuwa akiishi nyumba moja na Kato bado anatafutwa na polisi baada ya kukimbia
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment