KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, December 30, 2010

Mahakama yaingilia mchakato wa zabuni


MAHAKAMA Kuu Kanda ya Arusha, imeagiza Halmashauri ya Jiji la Arusha kusitisha mara moja kutoa zabuni ya kukusanya ushuru wa maegesho ya magari kwa Kampuni ya Piga Deal.

Uamuzi huo, ulitolewa na Jaji Kakusulo Sambu kutokana na kesi ya madai ya kupinga kutolewa zabuni hiyo, iliyofunguliwa na Kampuni ya Jamahedo Food Collection ambayo awali ilikuwa ikukusanya ushuru huo.

Akitoa uamuzi huo, Desemba 29, mwaka jana, Jaji Sambu aliagiza jiji kutoendelea na mchakato wa kutoa kazi ya kukusanya ushuru kwa Kampuni ya Piga Deal, hadi kesi ya msingi kupinga uamuzi wa zabuni hiyo itakaposikilizwa.
Kampuni ya piga Deal, ilipewa idhini ya kukusanya ushuru Januari Mosi, mwaka huu.

Hata hivyo, Jamahedo Food Collection kupitia wakili wake, Loom Oljare, ilipinga uamuzi huo kutokana na kukiukwa taratibu kadhaa ikiwemo Kampuni ya Piga Deal kushindwa kuweka dhamana ya zabuni ndani ya siku 21, na siku nyingine 14 za ziada.

Piga Deal ilipeleka malalamiko yake Mamlaka ya Rufani ya Zabuni Tanzania (PPAA), ambayo ilikubali maombi ya kampuni hiyo kupewa zabuni hiyo.

Katika uamuzi wa Jaji Sambu, Mahakama Kuu imeiagiza halmshauri ya jiji kusitisha uamuzi wa rufaa iliyowasilishwa na Kampuni ya Piga Deal namba 85/2010 na ule uliotolewa Desemba 14, mwaka huu na PPAA, kwani haukuzingatia sheria ilizojiwekea sanjari na sheria ya ununuzi ya PPRA

No comments:

Post a Comment