KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, December 30, 2010

11 Wafariki Wakisherehekea Mwaka Mpya Nigeria


Zaidi ya watu 11 wamefariki dunia nchini Nigeria kufuatia bomu kubwa lililolipuka kwenye baa wakati watu wakisherehekea mwaka mpya.
Zaidi ya watu 11 wamefariki dunia kufuatia bomu kubwa lililolipuka kwenye baa iliyopo karibu na kambi ya jeshi iliyopo karibu na ikulu mjini Abuja.

Eneo hilo lilikuwa likisemekana kuwa ndilo lenye usalama kuliko maeneo yote ya mji wa Abuja.

Wakati wa krismasi wiki iliyopita zaidi ya watu 80 walifariki dunia nchini Nigeria kutokana na milipuko ya mabomu katika mji wa Jos ambao umekumbwa na chuki ya kidini kati ya waislamu na wakristo.

Katika bomu lililotokea mkesha wa mwaka mpya, inakadariwa kuwa watu 30 wamepoteza maisha yao ingawa taarifa ya polisi ilithibitisha vifo vya watu 11.

Bomu hilo lilitokea muda mfupi kabla ya mwaka mpya wakati watu wakiwa wanajiburudisha baa wakisubiri kusherehekea mwaka mpya 2011.

Waziri wa ulinzi wa Nigeria amewataka watu wadumishe utulivu wakati uchunguzi mkali ukiendelea kuhusiana na milipuko ya mabomu ambayo imekuwa ikiiandama Nigeria siku za karibuni

No comments:

Post a Comment