KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, December 15, 2010

Machafuko ya baada ya Uchaguzi nchini Kenya.

Machafuko ya baada ya Uchaguzi nchini Kenya.
Tathmini kuhusu hatua ya ICC Kenya

Wawili kati ya wanasiasa waliotajwa Uhuru Kenyatta na mbunge wa Eldoret Magharibi William Ruto tayari wameelezea nia ya kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2012.

Iwapo majaji wa mahakama ya kimataifa wataidhinisha mashtaka dhidi yao, basi huenda mipango yao ikawa imesambaratika.

Japo Rais Mwai Kibaki na Waziri Mkuu Raila Odinga hawakutajwa, orodha iliyotolewa na bwana Moreno-Ocampo inawagusa kwa karibu viongozi hao wawili.


Machafuko ya baada ya Uchaguzi nchini Kenya.

Bwana Uhuru Kenyatta ambaye pia ni waziri wa fedha ni mwandani wa karibu wa Rais Kibaki ambaye baadhi ya wakazi wa mkoa wa kati anakotoka rais Kibaki, wamekuwa wakimwona kama aliye katika mstari wa mbele wa kuchukua wadhifa wa urais

Kiongozi wa mashtaka katika mahakama ya ICC Luis Moreno Ocampo.

Mbali na bwana Uhuru, bwana Moreno Ocampo ameonekana kumkaribia zaidi rais kwa kumtaja katibu wa baraza la mawaziri Francis Muthaura ambaye pia ni mkuu wa utumishi wa umma.

Bwana Muthaura ni mwandani wa tangu jadi wa Rais Kibaki.

Kutokana na wadhifa wake ambao unategemea zaidi amri ya Rais huenda Rais Kibaki akaona kutajwa kwa bwana muthaura kama kunaomgusa karibu mno.

Waziri mkuu Raila Odinga pia ameachwa akikuna kichwa baada ya mwenyekiti wa chama chake, ODM, Henry Kosgey kutajwa kama mmoja aliyepanga ghasia zilizotokea.

Isitoshe bwana Kosgey ndiye mwanasiasa mkuu wa eneo la Rift Valley ambaye ameendelea kumuunga mkono waziri mkuu hata baada ya wenzake wa eneo hilo kujitenga na bwana Odinga na kujiunga na kundi la aliyekuwa waziri wa elimu ya juu William Ruto.



Waziri Mkuu ambaye hapo awali alielezea kuunga mkono mahakama ya kimataifa sasa atakabiliwa na hali ngumu ya kuamua kama ataendelea kushikilia msimamo huo au atamtetea mkuruba wake.

Hivi juzi taarifa za siri za ubalozi wa Marekani zilizotolewa na tovuti ya wikileaks zilimnukuu balozi wa Kenya, Michael Ranneberger akiwataja Rais Mwai Kibaki na Waziri Mkuu Raila Odinga kama baadhi ya viongozi wanaopinga mabadiliko nchini Kenya na jamiii ya kimataifa sasa itakuwa ikitazama kwa makini jinsi viongozi hawa watakavyojiendesha baada ya waandani wao kutajwa na bwana Moreno OCampo

No comments:

Post a Comment