KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, December 15, 2010

Kura ya maoni Sudan: UN yakaza kamba

Jeshi la Sudan Kusini.


Baraza la usalama la umoja wa mataifa limeongeza shinikizo kwa Sudan Kaskazini na Kusini kuhakikisha kuwa kura ya maoni inayotarajiwa na wengi kwamba itapelekea kugawanywa kwa taifa hilo ambalo ni kubwa zaidi barani Afrika inafanyika kwa njia ya amani mwezi ujao.

Baraza hilo la usalama limetaka pande zote mbili-Kaskazini na Kusini-kutuliza hali ya wasiwasi inayozidi kuongezeka na kuafikia mkataba kuhusu kura tofauti-ya maamuzi juu ya mustakabal wa jimbo lenye utajiri mkubwa wa mafuta la Abyei.

Pande zote mbili-kaskazini na kusini zinadai umiliki wa jimbo hilo.

Umoja wa mataifa pia umeelezea wasiwasi wake kuhusiana na matukio kadhaa ya kijeshi katika siku za hivi karibuni ambao yamezidisha hali ya wasiwasi.

Kura hiyo itakayofanyika tarehe tisa mwezi januari inajiri baada ya mkataba wa amani wa mwaka 2005 ambao ulimaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu miongo miwili kati ya Kaskazini na Kusini.

No comments:

Post a Comment