KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, December 2, 2010

Jeshi lafunga mipaka Ivory Coast



Jeshi la Ivory Coast limefunga mipaka ya nchi hiyo na kuzuia vyombo vya habari vya nje huku hali ya wasiwasi ikizidi kuongezeka kuhusiana na matokeo ya raundi ya pili ya uchaguzi wa urais.



Hatua hiyo imekuja baada ya Mahakama ya Katiba kupinga matokeo yaliyotangazwa na tume ya uchaguzi kuwa mgombea wa upinzani Alassane Ouattara ameshinda.

Wafuasi wa Rais Laurent Gbagbo walijaribu kuzuia kutoka kwa matokeo hayo yaliyocheleweshwa, wakidai umefanyika wizi wa kura katika eneo la kaskazini.



Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa limetaka pande zote kuonesha uvumilivu.

"Mipaka yote, ya anga, ya ardhini na ya baharini imefungwa kwa watu na mizigo," amesema msemaji wa jeshi Babri Gohorou.

Mipaka hiyo itabaki katika hali hiyo mpaka tangazo lingine litakapotolewa, Bw Gohourou ameongeza.



Muda mfupi baadaye jeshi hilo lilitangaza "fungunga mara moja kwa matangazo ya vyombo vya habari vya kigeni" nchini humo ikiwemo CNN, France24 na Radio France International FM.

Tangazo la matokeo ya uchaguzi uliofanyika Jumapili, limecheleweshwa sana, na hivyo kusababisha kuwepo kwa hali ya wasiwasi nchini humo.

Wafuasi wa Rais laurent Gbagbo walijaribu kuzuia matokeo hayo kutoka, wakisema umefanyika wizi katika eneo la kaskazini ambapo Bw Ouattara ana umaarufu mkubwa.

Upande wa kaskazini unadhibitiwa na waasi wa zamani

No comments:

Post a Comment