KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, December 30, 2010

Itachukua muda kukarabati Queensland

Waziri mkuu mkuu wa jimbo la Queensland nchini Australia, Anna Bligh, ameonya itachukuwa miezi kadhaa kukarabati maeneo yaliyoharibiwa na mafuruko mabaya zaidi kukumba jimbo hilo.


Mafuriko Australia


Bi Bligh alikuwa akizungumza katika mji wa Rockhampton, ambao ni moja ya miji mikubwa ishirni na mitatu iliyozingirwa na mafuriko na misaada ya kibinadamu inasafirishwa kwa ndege za kijeshi.

Watu wawili wamekufa katika mafuriko hayo na maelfu wengine wameachwa bila makazi.

Maafisa wa jimbo hilo na serikali ya shirikisho, wameahidi kutoa misaada ya kutosha kuwasaidia wakulima pamoja na wafanyibiashara wadogowadogo walioathirika na mafuriko hayo.

Ndege za kijeshi zimekuwa zikipeleka misaada ya chakula na dawa, katika maeneo yaliyoathirika vibaya na mafuriko hayo katika jimbo la Queensland.

Mji wa Rockhampton umetengwa kutokana na mafuriko hayo kwa muda wa zaidi ya wiki moja.

Mwandishi wa BBC katika eneo hilo, ameeleza eneo hilo inaonekana sawa na kisiwa kidogo kilichozingirwa na maji huku mafuriko yakizidi kuongezeka
No comments:

Post a Comment