KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, December 15, 2010

Gwikama: Maandamano walemavu hayakuwa halali


Hamad Amour na Hemed Athuman (TSJ) MWENYEKITI wa shirikisho la vyama vya wafanyabiashara walemavu jijini Dar es salaam (Uwawada), Peter Gwikama amesema maandamano yaliyofanywa hivi karibuni na baadhi ya wanachama wa umoja huo, si halali.

Gwikama alisema kitendo cha wafanyabiashara hao, kuandamana na kufunga ofisi za chama zilizopo Buguruni jijini Dar es Salaam, sio njia sahihi ya kupata ufumbuzi wa madai yao.

Wafanyabiashara hao, walifanya maandamano kushinikiza uchaguzi mpya ufanyike kwa kuwa uongozi uliopo madarakani umemaliza muda wake.

“Njia pekee ya kupata ufumbuzi ni kufanyika kwa vikao vya chama na kufanya uchaguzi utakaothibitisha kiongozi yupi awe madarakani na yupi aondoke, lakini sio kwa migomo na maandamano,”alisema Gwikama.

Alisema uchaguzi huo, ulichelewa kufanyika kutokana na wafanyabiashara hao, kuhama mara kwa mara na kufafanua kwamba awali wafanyabiashara hao, walikuwa Mnazimmoja na baadaye kuhamishiwa Lumumba, baadae Karume na sasa wamehamishiwa Mchinga Complex Ilala.

Mmoja wa wajumbe wa chama hicho, Athuman Sembe alisema viongozi hao, viongozi hao wanakabiliwa na tuhuma za kuuza vizimba vya kufanyia biashara,vilivyotolewa kwa walemavu na kwamba kizimba kimoja walikuwa wakiuza kati ya Sh 100,000 hadi 600,000.

Naye Mwenyekiti wa umoja huo, alifafanua kwamba chama hicho, kilipewa vizimba 700 vya kufanyia biashara Machinga complex, na vizimba vyote viligawiwa kwa watu.

“Chama kinazaidi ya wanachama 1,200 kati ya hao waliopata nafasi ni wale walioandika barua na kujaza fomu za mkataba wa kumiliki vizimba hivyo na ambao hawajapata hawakujaza fomu za mkataba,” Alisema Gwikama

No comments:

Post a Comment