KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Thursday, December 30, 2010

CUF yaizidi ujanja Polisi


WAKATI Askari wa Kutuliza Ghasia wakitanda na magari yao katika maeneoya katikati ya jiji na wengi kuonekana kusubiri maandamano katika barabara ya Uhuru, wafuasi wa CUF walifanikiwa kuwasilisha rasimu yao kwa katibu mkuu wa Wizara hiyo
Askari polisi walikwua maeneo hayo kuzuia kutofanyika wka maandamano hayo ambapo agizo hilo lilitolewa na jeshi la polisi nchini kwa kuwa maandamano hayo hayakuwa ya halali.

Maandamano hayo yaliongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Bw. Julius Mtatiro na wapenzi mbalimbali kutoka ndani ya chama hicho, walifanikiwa kuingia barabarani na kuwasilisha rasimu yao ya katiba kama walivyopanga.

Maandamano hayo yayakuanza majira ya saa 2 kama yalivyopangwa kwa kuwa askari polisi walifika eneo la Buguruni sheli walipopanga kuanzia maandamano hayo na kuwatangazia watawanyike na kutangaza hatri endapo watakaidi matangazo yaliyosikika wka njia ya spika kutoka kwenye gari la polisi.

Baada ya tofauti hiyo kati yao na polisi punde ilipotimu majira ya saa 3:30 asubuhi, gari la matangazo la CUF lilipita na kutangaza kuwa maandamano yapo palepale na yataanzia Makao Makuu ya Chama hicho ifikapo, saa 4:30 asubuhi badala ya Buguruni Sheli.

Mara baada ya tangazo hilo, wananchi walianza kukusanyika tena kwa wingi nje ya makao makuu ya chama hicho wakiwa na mabango mbalimbali kuashriia kutaka katiba mpya yaliyobebwa na wafuasi wa chama hicho.

Vita ilianza kati ya weafuasi hao na askari polisi bada ya askari nao kautangaza hali ya hatari kuwataka wananchi hao watawanyike na kuwataka wakazi wa Karibu na eneo hilo waingie majumbani mwao, na kuwatangazia wafanyaiashara wafunge biashara zao na kuwatangzia waandishi wa habari kuondoka mahali hapo kani wanataka kuanza mapambano kati yao na wafuasi hao matangazo yaliyotolewa kwa njia ya vipaza sauti.


Wafuasi hao nao walionekana kukaidi agizo hilo na kuendela kuimba na kuonyesha mabango yao na wakisikika wakisema “Kama ni mabomu, maji ya kuwasha tumeshazoea hakuna cha ajabu hapa, huku wakisogelea magari hayo ya askari wa kutuliza ghasia.”

Vita kamili ilianza pale wafuasi hao walipofika eneo la Buguruni Malapa na kutakiwa wasiendelee na msafara na kuonekana kukaidi na ndipo gari la maji ya kuwasha lilipofunguliwa na kuanza kuwamwagia maji wafuasi hao na kuingia mitaani na askari polisi wakidhani watu hao wamekata tama na baadae maandano hayo yaliatokea na kufika eneo la Karume na ndipo askari hao waliposhtuka na kukimbia kufika eneo hilo kwa hsira na wananchi wakidhani picha na askari kuanza kurusha risasi za moto eneo hilo na mabomu ya hapa na pale

Hata hivyo juhudi za wafuasi hao zilzaa matunda baada ya kufanikiwa kuika katika ofisi za wizara hiyo na kumkabidhi rasimu hiyo Katibu Mkuu wa wizara hiyo .

Wakizungumza na nifahamishe mara baada ya kukabishi rsimu hiyo walisema “Tumefanikiwa kukabishi rasimu yetu, japo mandamano yeatu yalionekana kuwa magumu kama ulivyoona, lakini mandanao yetu yalikuwa ni halali kabisa”

“Japokuwa hatujamkuta waziri lakini tumeshamkabidhi Katibu na tunashukuru imepokelewa“ alisema Mtatiro.

Alihoji mwandishi wa habari hii kwa kuwa wahakupewa furusa ya kuingia ndani wakati wa makabishiano hayo

No comments:

Post a Comment