KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Wednesday, December 15, 2010

Breaking News - Abuu Semhando Afariki Dunia

Abuu Semhando aka Baba Diana
Mwanamuziki nyota wa bendi ya Twanga Pepeta, Abuu Semhando aka Baba Diana amefariki dunia usiku wa kuamkia leo kutokana na ajali ya pikipiki.
Abuu Semhando mwanamuziki nyota wa bendi ya African Stars Twanga Pepeta hatunaye tena baada ya kugongwa na gari wakati akiendesha pikipiki kwenye majira ya saa kumi usiku.

Umauti ulimkuta Semhando wakati akijerea nyumbani kwake akitokea kazini ambapo bendi ya Twanga Pepeta ilikuwa ikifanya shoo eneo la Africana Mbezi Beach.

Mmoja wa wanenguaji wa Twanga Pepeta, Queen Suzi akiongea na Nifahamishe.Com alisema kuwa alikuwa akitaniana na Semhando wakati akipiga tumba lakini hakuwa mchangamfu muda wote.

Msiba upo Mwananyamala nyumbani kwake

No comments:

Post a Comment