KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, December 10, 2010

..Australia yautetea mtandao wa Wikileaks

Wikileaks watetewa

Waziri wa mambo ya nje wa Australia, Kevin Rudd, amemtetea muasisi wa wavuti ya wikileaks raia wa Australia, Julian Assange, akisema Marekani ndiyo ya kulaumiwa kwa kufichuliwa kwa hati za siri.




Bwana Rudd amesema wale waliofichua siri hizo kwanza ndiyo wanaopaswa kuwajibika kisheria, wala siyo bwana Assange aliyechapisha.

Matamshi hayo yanaonekana kutofautiana na ya Waziri Mkuu wa Australia, Julia Gillard, ambaye amemshtumu Assange kwa kutokuzingatia maadili.

Muasisi huyo wa Wikileaks amezuiliwa na polisi jijini London akisubiri kusafirishwa.

Anatakiwa nchini Sweden kwa madai ya ubakaji, madai ambayo amekanusha.

Maafisa wa polisi nchini Sweden wanasema kukamatwa kwake hakuhusiani na siri alizochapisha kwenye mtandao wa Wikileaks

No comments:

Post a Comment