KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Thursday, December 2, 2010

Aishi na Maiti ya Mama Yake Kwa Mwezi Mmoja


Harufu kali iliyokuwa ikitoka kwenye nyumba moja nchini Macedonia ilipelekea kutiwa mbaroni kwa mwanamke mmoja nchini humo ambaye alikuwa akiishi na maiti ya mama yake kwa zaidi ya mwezi mmoja.
Majirani wa nyumba moja katika mji mkuu wa Macedonia, Skopje, walilazimika kuwaita polisi baada ya kushindwa kuvumilia harufu mbaya iliyokuwa ikitoka kwenye nyumba hiyo.

Polisi walipoingia ndani ya nyumba hiyo walishangazwa kuiona maiti ya bibi Anastasiya Karamanova ambaye alifariki mwezi mmoja uliopita akiwa na umri wa miaka 82.

Mtoto wake wa kike mwenye umri wa miaka 42 ambaye alitajwa kwa jina la Rozita, alikuwa akiishi kwenye nyumba hiyo.

Rozita alikuwa akiendelea na maisha yake kama kawaida, akitoka asubuhi kwenda shughuli zake na kurudi jioni na hakuwahi kutoa taarifa ya kufariki kwa mama yake kwa mtu yoyote ile.

Kugunduliwa kwa maiti ndani ya nyumba hiyo kumewafanya polisi waamue kumfanyia uchunguzi wa akili Rozita ili kujua amewazaje kuishi kwenye nyumba hiyo pamoja na maiti ambayo ilikuwa imeharibika vibaya sana.

Rozita ndiye mshukiwa namba moja wa kifo cha mama yake baada ya polisi kugundua alama za kipigo kwenye mwili wa mama yake

No comments:

Post a Comment