KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, November 10, 2010

Viongozi wa Iraq watafuta maridhiano



Mkutano wa ngazi ya juu umeanza nchini Iraq, kutafuta mbinu za kufikia makubaliano ya kuundwa kwa serikali mpya kabla ya kikao cha bunge kufanyika Alhamisi ijayo.

Iraq imekuwa bila serikali tangu uchaguzi wa ubunge kufanyika mwezi machi.


Waziri mkuu wa sasa, Nouri Al Maliki, na mpinzani wake mkuu, Iyad Allawi ni miongoni mwa viongozi wanaoshiriki katika mazungumzo hayo.



Akifungua rasmi mkutano huo, kiongozi wa wa-Kurdi, Masoud Marzani, ambaye aliongoza mashauriano hayo yanayonuia kutafuta mwelekeo wa kuunda serikali mpya nchini humo, amesema kuwa kufanikisha kuwaleta pamoja viongozi hao ilikuwa ni ufanisi wa kitaifa.




Nouri Al Maliki ambaye huenda akasalia kama waziri mkuu wa nchi hiyo, naye amesema kuwa ukurasa mpya umefunguliwa katika kutafuta usalama na maendeleo nchini humo.





Lakini, Iyad Allawi, ambaye alimshinda Nouri Al Malaki kwa kura chache, alisisitiza umuhimu wa kugawana madaraka kwa njia ya haki, ikiwa ni pamoja na upande wao kujumuishwa katika shughuli za maamuzi muhimu.

Hiki ni kikao cha a kwanza kwa viongozi wote nchini Iraq , tangu uchaguzi mkuu kufanyika zaidi ya miezi minane iliyopita

No comments:

Post a Comment