KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Tuesday, November 9, 2010

Aliwa na Simba Wakati Akioga Porini


Mfanyabiashara mmoja wa nchini Zimbabwe ameliwa na Simba wakati akioga chini ya mti kwenye pori aliloweka kambi pamoja na watalii wenzake.
Peter Evershed akiwa na mkewe pamoja na watalii wengine aliweka kambi porini baada ya tripu ya kuvua samaki katika mji wa Chitake mpakani mwa Zimbawe na Zambia.

Mfanyabiashara huyo mwenye umri wa miaka 59 aliuliwa na kundi la simba waliomzunguka na kumshambulia wakati akioga usiku chini ya mti uliokuwa karibu na kambi waliyoweka.

Kwa mujibu wa msemaji wa polisi wa Mashonaland, Peter alipiga kelele kuomba msaada toka kwa watalii wenzake lakini simba hao waliendelea kumshambulia.

"Alipiga kelele kuomba msaada toka kwa watalii wenzake ambao waliwamulika simba hao na taa ili kuwakimbiza lakini simba hao waliendelea kumshambulia".

Simba waliendelea kumshambulia hadi mkuu wa msafara huo alipopiga risasi hewani na kuwafanya simba wakimbie.

Lakini hadi wakati huo, Simba hao walikuwa wameishamjeruhi vibaya sana Peter na kupelekea kifo chake, liliripoti gazeti la Herald Online la nchini humo

No comments:

Post a Comment