KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, November 19, 2010

SAP yatozwa bilioni kwa kuiba siri

Kampuni moja ya Ujerumani ya masuala ya Kompyuta SAP imeamrishwa kutowa takriban dola bilioni moja nukta tatu kwa kuiba siri za Kampuni nyingine
Mtambo wa kompyuta kabambe

Wanasheria wa kampuni hiyo ijulikanayo kama Oracle, wamesema kuwa adhabu hiyo ndiyo kubwa kuwashi kuwasilishwa katika kesi inayohusiana na utumiaji haramu wa hati miliki. Hicho ndiyo kiwango kilichoafikiwa na jopo la mahakama baada ya majuma matatu ya kusikiliza kesi hiyo.

Halikadhalika uwamuzi huo umeonekana kuwa pigo kwa sifa na heshima ya mojapo ya kampuni zinazotowa huduma katika biashara ya vifaa vya kopyuta duniani.

SAP daima imekiri kuwa mojapo ya matawi yake iliyokuwa ikijulikana kama TomorrowNow -iliyotoweka ilinakili vifaa vya Oracle kupitia mtandao kwa ajili ya matumizi yake na kuwavuta wateja wa Oracle


SAP inadaiwa kuibia vifaa na wateja wa Oracle


Hata hivyo SAP imesema kuwa athari ya adhabu ya malipo ni ndogo sana na imedai iko tayari kulipa hadi milioni 40 badala ya bilioni na nukta tatu.

Halikadhalika jopo linaonekana kuafikiana na hoja ya Oracle kuwa kiwango cha athari kizingatiwe na kuonyesha thamani ya leseni endapo SAP ingetakiwa kununua leseni kwa bei ya juu ili iweze kutumia vifaa vya Kompyuta ilivyotumia kinyume na utaratibu wa sheria.

Bila shaka adhabu hiyo ndiyo kubwa kuwahi kutozwa katika kesi baina ya makampuni. Mawakili wa Oracle wamekubali kuwa hiki ni kiwango kikubwa kuwahi kutozwa.

Wakuu kutoka kampuni zote mbili walitoa ushahidi katika kesi hii kwa kipindi cha majuma mawili, ikijitokeza kuwa hadithi iliyovutia wengi katika eneo la Silicon Valley huko Carlifornia, kitovu cha viwanda vya teknolojia ya juu.

SAP, Oracle na kampuni nyingine Hewlett packard zinahusika katika mvutano wa kumiliki soko kubwa la kopyuta linalokadiriwa kua na thamani ya mabilioni ya dola.

Kwa sasa SAP iliyomiliki nyanja hiyo ya kutoa huduma za vifaa vya kopyuta inakabiliwa na kitisho kutoka kampuni hizo mbili.

Pamoja na hayo kesi hii imefichua kwamba kuna athari za ujasiri wa kuibia siri za kampuni mwenza

No comments:

Post a Comment