KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Monday, November 1, 2010

Mtuhumiwa Guantanamo ahukumiwa miaka 40


Omar KhadrMahakama ya kijeshi katika gereza la Guantanamo Bay imemhukumu kijana moja mpiganaji wa kundi la kigaidi la , kifungo cha miaka arobaini jela baada ya kupatikana na makosa ya mauaji na ugaidi.


Lakini kutokana na jinsi alivyojitetea, Khadr atatumikia kifungo cha miaka minane pekee.

Omar Khadr alikamatwa nchini Afghanistan mwaka wa 2002 akiwa na umri wa miaka kumi na mitano, wakati wa mapigano makali ya risasi kati ya wanajeshi wa Marekani na wapiganaji wa Kiislamu.

Mshukiwa huyo alikiri mashtaka dhidi yake yakiwemo mauaji ya mwanajeshi mmoja.

Marekani imesema mshukiwa huyo atarejeshwa nyumbani kwao nchini Canada baada ya kutumikia kifungo cha mwaka mmoja gerezani nchini humo.

No comments:

Post a Comment