KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, November 1, 2010

Brazil yapata Rais mpya ni Dilma Roussef



Dilma Roussef


Mgombea wa chama tawala cha Workers party nchini Brazil, Dilma Roussef amechaguliwa kuwa rais mpya wa nchi hiyo na kuandikisha historia ya kuwa mwanamke wa kwanza kuongoza taifa hilo.


Bi Roussef alishinda asilimia 56 ya kura zote zilizopigwa dhidi ya mpinzani wake wa chama cha Social Democrat Jose Serra katika duru hiyo ya pili ya uchaguzi wa urais.

Mwanamama huyo amehaidi kutimiza ahadi alizotoa wakati wa kampeini na pia kuendeleza sera zitakazopunguza viwango vya umaskini nchini humo.

Bi Rossef aliungwa mkono na rais wa nchi hiyo anayeondoka madarakani Luis Inancio da Silva

No comments:

Post a Comment