KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, November 11, 2010

Mateka 19 wakombolewa Niger Delta



Waasi wa MEND nchini Nigeria
Kikosi maalum cha kijeshi nchini Nigeria, kimevamia kambi mbili za wanamgambo nchini humo na kuwachilia huru mateka 19 katika eneo la Niger Delta.

Duru kutoka idara ya usalama zinasema ilikuwa operesheni kubwa ya anga, nchi kavu na majini ambayo ilitekelezwa na majeshi ya Nigeria.

Uvamizi huu wa kijeshi unaadhimisha mabadiliko ya mbinu za kijeshi nchini Nigeria, katika kukabiliana na machafuko ya hivi majuzi katika eneo la Niger Delta.

Operesheni hii ni ya kwanza kufanikiwa kuwakomboa mateka wa kigeni katika eneo hilo lenye utajiri mkubwa wa mafuta, bila ya mateka yeyote kuuwawa.

Inaaminika kuwa raia 12 wa Nigeria waliokolewa katika operesheni hiyo ya Kijeshi.

Mateka wa kigeni waliokombolewa ni wawili kutoka Marekani, wawili wa Indonesia, Wawili kutoka nchi ya Ufaransa na mmoja raia wa Canada.

Inasemekana kuwa wote wako salama, kufuatia operesheni hiyo ya kuogofya.

Ufanisi wa uvamizi huo umetokana na ushirikiano kati ya wanajeshi wa Nigeria na wakaazi katika eneo la Niger Delta.

Bado sio wazi kama kuna mwanachama yeyote wa kundi la wanamgambo aliuwawa au kujeruhiwa

No comments:

Post a Comment