KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Thursday, November 11, 2010
DRC yaondelewa madeni yake ya $7B
Jamii ya kimataifa imefutilia mbali madeni ya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inayokisiwa kuwa zaidi ya dola billioni saba.
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ilikuwa ikidaiwa pesa hizo na kundi la mataifa 19 yanayofahamika kama kundi la Paris club.
Kundi hilo sasa limetoa wito kwa serikali ya DRC, kuimarisha uongozi na kupambana na ufisadi nchini humo.
DRC inatarajiwa kutoa ombi sawa na hilo ili madeni yake yaliyosalia yafutiliwe mbali. Nchi hiyo imehaidi kutumia pesa zitakazopatikana baada ya madeni hayo kufutwa kwa miradi ya kupunguza umaskini nchini humo.
Madeni hayo yamefutiliwa mbali baada ya Benki Ya Dunia na shirika la fedha duniani IMF kutia saini mkataba mwa mkopo wa dola bilioni nane kwa nchi hiyo.
Hata hivyo mashirika hayo yameelezea wasi wasi wao kuhusu hali ya uwajibikaji na uwazi katika serikali ya nchi hiyo na pia mazingira ya kufanyia biashara nchini Congo.
Jean-Louis Kayembe, mkurugenzi mkuu wa kamati inayohusika na masuala ya sera za kiuchumi katika benki kuu ya Congo, amesema, hatua hiyo inamaanisha kuwa madeni ya serikali ya Congo sasa itapungua kwa 82.4%.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment