KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, November 11, 2010

Maharamia wateka meli ya Wachina


Maharamia wa Kisomali


China imesema maharamia wameiteka meli ya mizigo katika bahari ya Uarabuni iliyobebea mabaharia 29 raia wa China.
Vyombo vya habari vya serikali ya China vimesema wamiliki wa meli hiyo yenye usajili wa Panana, walisema meli hiyo ilikuwa ikielekezwa upande wa Somalia na maharamia hao.

Shirika la Kimataifa la Shughuli za Bahari, limesema maharamia Wakisomali wanashikilia meli ishirini zikiwa na wafanyakazi zaidi ya mia nne wakitaka kulipwa fedha za kikombozi

No comments:

Post a Comment