KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, November 11, 2010

Msikate tamaa - Suu Kyi

Kiongozi wa harakati za kidemokrasia nchini Burma, Aung San Suu Kyi amewataka wafuasi wake kutokata tamaa, ikiwa ni siku moja baada ya kachiliwa huru.



Bi Suu Kyi akiwasili kwenye makao makuu ya chama chake


"Hakuna sababu ya kukata tamaa," amewaambia maelfu ya watu waliokusanyika nje ya makao makuu ya chama chake cha siasa mjini Rangoon.

Bi Suu Kyi aliachiliwa huru na jeshi baada ya kifungo chake kufikia kikomo siku ya Jumamosi.

Viongozi mbalimbali duniani na makundi ya haki za binaadam yamefurahia hatua ya kuachiwa huru kwa Suu Kyi.

Bi Suu Kyi amekaa kizuizini kwa miaka 15 katika kipindi cha miaka 21 iliyopita, ikiwa ni kifungo cha nyumbani, au gerezani.

Rais wa Marekani Barack Obama amefurahishwa na hatua hiyo pia akisema "ilitakiwa kufanyika siku nyingi",

huku katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akisema Bi Suu Kyi ni "hamasa" na kuitaka Burma kuwaachilia huru wafungwa 2,200 wa kisiasa.

No comments:

Post a Comment