KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, November 3, 2010

China yakataa pendekezo la MarekaniChina yakataa pendekezo la Marekani
China imekataa pendekezo la Marekani kuandaa mazungumzo ya nchi tatu na Japan kuutanzua mzozo unaozunguka umiliki wa visiwa kadhaa katika bahari ya mashariki ya China.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China amesema mzozo huo unapaswa kutatuliwa na nchini hizo mbili bila kuishirikiwa Marekani.

Wazo hilo lilitolewa na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bi Hillary Clinton wakati wa mkutano wa viongozi wa serikali za nchi wanachama wa muungano wa mataifa ya mashiriki mwa bara Asia uliofanyika Vietnam.

Uhasama kati ya China na Japan umeongezeka tangu wanamaji wa Japan walipomkamata nahodha wa meli moja ya uvuvi karibu na visiwa hivyo mwezi Septemba mwaka huu

No comments:

Post a Comment