KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, October 13, 2010

Wanawake Watatu Wambaka Mwanaume ZimbabweWanawake watatu wanatafutwa na polisi nchini Zimbabwe baada ya kumteka mwanaume na kisha kumbaka kabla ya kumtelekeza pembeni ya barabara baada ya kumuibia pesa zake.
Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 26 wa nchini Zimbabwe amebakwa na jumla ya wanawake watatu ambao walimteka baada ya kumlewesha kwa madawa ya kulevya.

Polisi wa Bulawayo walitoa taarifa ikisema kuwa mwanaume huyo aliwekewa madawa ya kulevya kwenye kinywaji chake na alipopoteza fahamu wanawake hao waliifunga na kamba mikono yake na kuondoka naye.

Mwanaume huyo aliripotiwa na polisi akisema kuwa wanawake hao walimbaka mara kadhaa na baadae kumtelekeza pembeni ya barabara baada ya kumuibia kiasi cha dola 300 alizokuwa nazo mfukoni.

Tukio la kubakwa kwa mwanaume huyo kumepelekea idadi ya wanaume waliobakwa mwaka huu wafikie watano

No comments:

Post a Comment